SEMINA KWA AJILI YA WAZEE WA KANISA

  

KANISA LA WAADVENTISTA WASABATO

NORTH EAST TANZANIA CONFERENCE

SEMINA KWA AJILI YA WAZEE WA KANISA

MTAA WA MUHEZA

Pr. Almodad Amos E-mail: Phone no: Website:

2 Pr. Almodad Amos

  Semina Fupi kwa Mzee wa kanisa

Asante kwa kuhudumu ukiwa kama Mzee wa kanisa mahalia popote ulipo. Kanisa lako

limekupatia majukumu yatakayohitaji maombi muda, juhudi, uvumilivu na wakati mwingine

hekima ya Sulemazi. Ikiwa unahisi kuwa na hofu hiyo ni hali ya kawaida kabisa.anguka

magotini na umgeukie Mungu. Yeye anatawala na atakutumia ikiwa ataruhusiwa kufanya hivyo.

Kabla hujaanza kuhudumu, nivizuri kuyajua majukumu yako na mamlaka ya kiblia

inayojenga hitaji la Mzee wa kanisa katika kanisa. Huu mwongozo umetengenezwa ili

ukufahamishe kazi na majukumu yam zee wa kanisa. Kwa nyongeza, utakuwa na wakati

mzuri wa kuyatazama makujumu yako ktk jamii utakayoiongoza na utaona ni jinsi gani unaweza kutimiza mahitaji ya wanafamilia wa kanisa unaloliongoza

Kazi a uzee wa kanisa na ichukuliwe katika hali ya kawaida. Biblia inatupatia maelekezo

mahususi juu ya majukumu na kujiweka wakfu juu ya kazi ya uzee wakanisa, na kile

ambacho Mungu anatarajia kwa wale wanaowekwa kusimamia nafasi hii. Hii si aina ya kazi

ambayo inakutaka tu uonekane kila sabato asubuhi kuwaita watu kuleta sadaka, au

umtambulishe muhutubu, inahitaji ujitoe kikamilifu katika muda wako binafsi. Kazi hii

inamuhitaji mtu aliyeamua kwelikweli, makubaliano baina yako na wale unaowaongoza

pamoja na usri mkubwa katika baadhi ya mambo makubwa yatakayolihusisha kanisa na waumini wake.

Unapoendelea kujifunza mwongozo huu, unaweza kujenga hitaji la kutaka kujua Zaidi na

zaidi. Utaweza kupata ufafanuzi Zaidi katika Mwongozo wa kanisa la Waadventista Wasabato (Kanuni ya kanisa) na Kitabu cha wazee wa kanisa la Waaventista Wasabato. Hivi

vinapatikana katika maduka ya vitabu ya ABC. Kama Mzee wa kanisa lazima ujifunze na

kuelewa utume wa kanisa lako, kazi zako na muundo wa uongozi pamoja na ngazi zake katika kanisa la Waadventista Wasabato.

Asante kwa utayari wako wa kuhudumu kwa uwezo uliopewa. Kumbuka kumuomba Mungu

ili akuongoze unapokua ukiwaeleza wengine juu ya upendo wake na kafara yake aliyoitoa ili tuupate uzima wa milele. N o r t h E a s t T a n z a n i a C o n f e r e n c e 3 | Biblia Inasema nini juu ya wazee wa kanisa?

Katika agano la kale, neno Mzee linamaana Zaidi ya mtu aliye na umri mkubwa sana;

inaweza pia kuwa mtuambaye amefikia kiwango flani cha utu uzima, uzoefu na hekima. Kwa

ujumla, neno Mzee linasimama kwa jili ya mtu ambaye ni kichwa cha familia au ukoo.

  

Mungu alipouumba ulimwengu, aliweka pia namna flani za uongozi katika jamii ya watu

wake. Katika nyakati za Ibrahimu, Isaka na Yakobo, Mungu alitumia mfumo wa wazee kama

msingi wa usimamizi wa ibada katika familia. Alitoa maelekezo ambayo yako wazi kabisa juu

ya utoaji wa kafara na kile zilichowakilisha.

  

Kadri vizazi vilivyoendelea kusogea, Mungu aliwaita watu wake kutoka katika nchi ya

utumwa na kwenda nchi ya ahadi. Katika kipindi hiki, Wana wa Israeli waliitwa kushuhudia

upendo wa Mungu na ahadi zake za kweli.

Hata hivyo Mungu alikua amemchagua Musa kuwa kiongozi wa kundi na kuwatoa Misri,

hata hivyo ilionekana kwamba ugawaji wa majukumu ktk kazi ni jambo ambalo linaongeza

ubora wa kazi. Jethro, Baba mkwe wa Musa, alionyesha hekima na uzoefu alipomwambia

Musa

  , “maana jambo hili ni zito mno kwako; huwezi wewe kulitenda peke yako. Utajipatia

katika watu hawa watu walio na uwezo, wenye kumcha Mungu, watu wa kweli, wenye

kuchukia mapato ya udhalimu; ukawaweka juu yao, wawe wakuu wa maelfu, na wakuu wa

mia, na wakuu wa hamsini, na wakuu wa kumi; nao wawaamue watu hawa sikuzote; kisha,

kila neno lililo kubwa watakuletea wewe, lakini kila neno dogo wataliamua wenyewe; basi

kwako wewe mwenyewe utapata nafasi zaidi, nao watauchukua huo mzigo pamoja nawe.

Kwamba utafanya jambo hili, na Mungu akikuagiza hivyo, basi utaweza kusimama wewe, na

watu hawa wote nao watakwenda mahali pao kwa amani.

  ” (Kutoka 18: 17, 21-23).

Kisha Bwana akamwambia Musa, “Nikusanyie watu sabini, miongoni mwa wazee wa israeli,

ambao wewe wawajua kuwa ndio wazee wa watu hawa, na maakida juu yao; ukawalete hata

hema ya kukutania, wasimame huko pamoja nawe. Nami nitashuka niseme nawe huko, nami

nitatwaa sehemu ya roho iliyo juu yako na kuiweka juu yao; nao watachukua mzigo wa watu

hawa pamoja nawe, ili usiuchukue wewe peke yako. ” (Hesabu 11:16, 17). Katika agano jipya, neno lililosimama kwa nafasi hii lilikua Mzee, askofu na mwangalizi . “Na

walipokwisha kuwachagulia wazee katika kila kanisa, na kuomba pamoja na kufunga,

wakawaweka katika mikono ya Bwana waliyemwamini.

  ” (Matendo 14:23 NIV). Baada ya haya aliwaacha waingie shambani kwa ajili ya kazi

Kwa kweli, baada tu ya kufa na kufufuka kwa Yesu, Mungu aliwaita tena watu wake kwa

mara nyingine, safari hii wayahudi na wayunani, kuwa jamii moja ya waumini. Wakati huu

pia alitoa maelekezo juu ya nafasi na majukumu ya viongozi.

Mafungu haya yanaonyesha jinsi kulivyo na hitaji la watu wa Mungu kuwafanya kazi pamoja

tena utaratibu mzuri. Kiongozi wa kanisa hutoa uongozi wa kiriho kwa jamii inayoliunda

kanisa, na pia humsaidia mchungaji kutimiza majukumu ya huduma za kiroho na kijamii pia.

Na katika haya ni vizuri kiongozi aungwe mkono na wale wanaomchagua.

4 Pr. Almodad Amos

  Semina Fupi kwa Mzee wa kanisa

Wazee katika Historia ya Kanisa la Waadventista Wasabato

Kanisa la Waadventista Wasabato liliiweka nafasi ya oungozi wa wazee mapema katika historia

yake. Jamii ya kwanza ya waumini walichagua mashemasi tu, lakini hili lilibadilika mwaka 1861.

  

Baada ya kujifunza kwa umakini, viongozi wa kanisa walitamka kwamba, muundo wa wazee wa

kanisa na mashemasi ulikua ni muundo wa kibiblia.

katika Muundo wa kanisa la Waadventista Wasabato, ikiwa kanisa halijapewa mchungaji wa

kanisa au mtaa na Konferensi, Mzee wa kanisa atatimiza mahitaji ya kichungaji katika kanisa

mahalia, ikiwa ni pamoja na kutembelea, kuhubiri, uinjilisti pamoja na maswala ya kiutawala.

  

Kunapokua na hitaji la kuamua kufanya kazi flani makini, Mungu huchagua

wanaume na wanawake kuifanya kazi yake, na ndipo itaonekana hasara ikiwa

talanta zao hazitaunganishwa.

  

(Evangelism, Uk 469)

SIFA ZA MZEE WA KANISA

  

Ili kibaraza kidogo kimchague mtu katika nafasi ya uzee wa kania, kuna vigezo muhimu sana vya

kuangali. Vigezo hivi ni pamoja na:

  1. Ajitoe kikamilifu kwa Mungu na kwa kuwatumikia wengine.

  2. Kuwa na uhusiano unaokua baina yake na Yesu. Hali yako ya kiroho si jambo linalojitokeza kila asubuhi ya sabato tu unapotaka kwenda kanisani.

  3. Pamoja na kuwa tayari kuutumia muda wako; unatakiwa kuweka uwiano katika mambo ya kanisa, familia na ajira yako binafsi. Utatakiwa kuwa na muda wa masaa 2 – 4 katikati ya juma ukikamilisha majukumu yako ya uzee wa kanisa.

  4. Hutakiwi kuongea kinyume na kanisa, na kinyume Imani za msingi, kinyume na viongozi wako na kinyume na

taratibu za kanisa. Uongozi wako wa mambo ya kiroho ujengeke juu ya Yesu Kristo na katika Biblia.

  5. Hakikisha kuwa tabia za wanafamilia zinaaksi uhusiano wako na Kristo 6. Usionekane hata kidogo kuhusika na aina yoyote ya zinaa (ikiwemo na ponography). N o r t h E a s t T a n z a n i a C o n f e r e n c e 5 | 7. Ukijua kuwa Mungu aliwaumba na

  Sifa za Mzee wa kanisa anawapenda wanadamu wote wasa. Kama watu tunaomuaksi hatuna la kufanya isipokua 1.

   Uhusuano binafsi na unaokia baina yako na . kuwapenda watu wote kwa usawa kristo.

  2.

  8. Anachaguliwa na kuwekwa madarakani na Kurudisha zaka kwa uaminifu na kuiungamkono kazi ya utume kwa michango kanisa mahalia. mbalimbali, kwa banisa mahalia na kimataifa 3.

   Anaheshimika sana na analiunga kanisa mkono pia. pamoja na mafundisho yake makuu.

  9. Kiri dhambi na makosa yako. Kuwa kiongozi 4.

   Anazosifa za uongozi na utawala muwazi na mfano kwa kanisa lako.

  5. Awe tayari kutuia muda na talanta 6.

   Awe na unyenyekevu wa mtumwa, ajue kuwa 10.

   Kuwasuluhisha waumini penye migogoro na watu wote ni sawa. hata uongozi pia. Unaliweza hili ikiwa tu utajenga mahusiano na waumini pamoja na kuwaombea. Kazi za Mzee wa kanisa Majukumu ya kiutawana na Uongozi wa Mzee wa kanisa Wazee wataitwa kuhudumu katika shughuli Wazee ni sehemu ya timu inayojumuisha, mbalimbali za kanisa. Hii ni pamoja na: baraza la wazee, baraza la kanisa na o Uongozi na utawala wa kanisa mahalia maofisa wa kanisa. Timu hii inasimamia na pia kutumia karama za roho. majukumu yote ya kanisa na hata utendaji o Kuliongoza kanisa katika uinjilisti wa shughuli za kikanisa. Wazee husaidia katika kutoa njizi za kanisa na katika unaolifanya kanisa likue. utekelezaji wa utume wa kanisa katika o

  Kuhakikisha kwamba waumini wapya jamii. wanatunzwa kiroho na kimahusiano pia.

  Kushiriki ktk vikao ni moja tu kati ya o Kuongoza huduma za ibada majukumu yam zee wa kanisa. Wazee wote o ni sharti wahudhurie vikao vya baraza la

  Kuhubiri o kanisa, na halimashauri za kanisa zima.

  Kutembelea Kwa nyongeza, wanaweza kuombwa o Kushiriki katika vikao vya kanisa kuhudumu katika baadhi ya kamati o Kudumisha ushirikiano wa mchungaji zinazowekwa na kanisa mahalia. na Mzee wakanisa o Kuandaa washiriki ili wawe

  Wazee wa kanisa wakutane na mchungaji mara moja kwa mwezi ili viongozi wazuri baadae kufanikisha utendaji wao kama timu moja, kuangalia maendeleo ya utendaji wa kazi na kuhakikisha kila jambo linakwenda kama lilivyopangiliwa

6 Pr. Almodad Amos

  Semina Fupi kwa Mzee wa kanisa

Katika kamati hizi, Mzee anakua na fursa ya kuwasaidia washiriki kuboresha huduma za

kiinjilisti kwa jamii. Kama Mzee, ni lazima uwe na uelewa wa uongozi wa kanisa. Tambua

majukumu ya viongozi wenzako kama karani wa kanisa, muhazini, shemasi, huduma binafsi,

shule ya sabato, nk.

  Nidhamu Ya Kanisa

Kwa kuwa tunaishi katika ulimwengu wa dhambi, inatulazimu kuwa na taratibu za

kinidhamu kanisani. Elewa kwamba nidhamu ni jambo la muhimu sana ili kudumisha

uadilifu wa waumini na kulifanya kanisa kuwa bora. Kama Mzee ni lazima utambue

hatua mbalimbali za kinidhamu, ikiwemo kumpa mtu karipio na kumfuta mtu ushirika.

  

Kumbuka kuwa utahusika sana na mambo ya watu binafsi, nay a siri ambayo

yanatakiwa kubaki katika usiri wake. Utatakiwa kuhusika na wazee wengine katika

maombi pale utakapo kabiliana na maamuzi magumu ya kuishughulikia dhambi kwa

mujibu wa biblia na katika hali ya upendo mwingi. Kumbuka kwamba: kushindwa

kumwadhibu mtu inaweza kumpeleka mbali na Mungu wake kuliko kama

ungelimwadhibu mtu huyo.

  Kuweka Mikakati

Kanisa linapokua na njozi ya mpango mkakati wa muda mrefu kwa jamii, inawasaidia

kuweza kuanzisha huduma mbalimbali na shughuli za kiinjilisti zitakazowaleta watu kwa

Yesu. Wazee husaidia kupangilia hii mikakati. Mpango mkakati kwa mwaka uzingatie mambo yafuatayo kwa umakini mkubwa: 1.

  Uinjilisti – Kanisa lako litafanya nini kueleza juu ya kisa cha ukombozi mwaka huu? Je,

  mtakua na majuma kadhaa ya mikutano ya injili? Je, washiriki watafundisha masomo ya Biblia? Je, shabaha yako ni watu wa kundi flani au umri flani? Utawezaje kufanikiwa kuifikia jamii yako kiinjilisti?

  2. Malezi – unapopangilia uinjilisti, usisahau kwamba unatakiwa kuwa na malezi kwa washiriki na waumini wapya katika familia ya kanisa lako. Utafiti unaonyesha kwamba washiriki wapya ni lazima wapate marafiki sita katika kipindi cha miezi sita ya kwanza ya ubatizo, vinginevyo watarudi tena nyuma.. kumbuka kulitangaza hili kila mara mtu anapobatizwa au anapopokelewa katika ushirika. Uwe na mkakati mapema kabisa wa kuwalea na kuwatunza washiriki wapya kabla hawajajitokeza. Tafakari yafuatayo: je kanisa lako linahitaji kamati ya malezi ya waumini? Je, utawapaia (washiriki wapya) walezi? Utahakikishaje kwamba mzunguko wa marafiki wao kanisani unakua? Pamoja na kuwalea waumini wapya, kanisa lako ni kwavipi litawafikia washiriki wa muda mrefu kanisani? Je, unampango wa kuwatembelea waliorudi nyuma, wasiojiweza, wagonjwa na wasiohudhuria kanisani? Je, utafanya nini kukidhi mahitaji ya watu walio katika jamii yako, kwa mfano wazazi wasioishi na wenzi wao, wasio na kwao, watoto wa mitaani? Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia washiriki wapya waliohamia katika kanisa lako kupata ushirika au kuhamisha ushirika wa walioondoka muda mrefu?

3. Vijana

  • – hii ni sehemu muhimu sana ya kuandaa na kutayarisha kanisa la kesho. Fanya kazi na vijana na uhakikishe unawaunga mkono, usiwapuuzie wala kuwapa kazi wasizoweza kumaliza. Uwe wakili wao katika kupanga bajeti ya kanisa. Kuza urafiki wako na vijana katika kanisa lako. Tambua majina yao na kile wanachopenda. Uwaunge mkono na

  7 | N o r t h E a s t T a n z a n i a C o n f e r e n c e

  kuwaacha wapangilie mambo mazuri katika nafasi za uongozi wao, katika huduma zao ili wakuze ujuzi wa taaluma ya uongozi.

  4. Wanafunzi wa vyuoni – hakikisha unawatambua wanafunzi vya vyuoni na unawajali. Ikiwa unawanafunzi ambao wanakwenda katka vyuo vya mbali na nyumbani, je, kama kanisa mnawatumia ujumbe kwamba kuonyesha umuhimu wao?

  • Washirki wapya waliobatizwa
  • Wazazi walioachana na wenzi wao
  • Wasio na watoto
  • Watu walio katika wakati mgumu
  • Wastaafu • Wafungwa • Wasiohudhuria • Wahitimu • wanafamilia wapya
  • Wanafunzi wa vyuoni Watoto na vijana ambao wanaweza wasiwe na mtu wa kuwatia moyo nyumbani kwa mambo ya kiroho

  Mnaweza kuwa na utaratibu wa kuhakikisha wanapata miongozo ya kujifunzia Biblia, na matoleo mengine kutoka kanisani. Uwaalike kushiriki uzoefu wao chuoni wanaporejea (Watoe huduma). Tafuta namna ya kuwashirikisha katika shugnuli za kanisa, wanaporejea nyumbani

  Je, kuna wanafunzi wanaosoma vyuo vya serikali karibu na wewe? Ikiwa ni hivyo, je, unakidhi mahitaji yao? Wako mbali na nyumbani, na wangependa kushiriki chakula cha nyumbani, je mnawajali angalau hata kwa hilo?

  Makundi ya kulea ( Wanaosahaulika ):

8 Pr. Almodad Amos

  Semina Fupi kwa Mzee wa kanisa Wanafunzi Waadventista katika vyuo hasa vya serikali, wanakumbana na changamoto za kufanya kazi Ijumaa jioni na siku ya sabato. Na mara nyingi mabweni yao na mazingira yao si mazuri sana kwa utunzaji wa sabato. Je, kuna namna ambayo kanisa lako laweza kuleta tofauti kwa ajili ya hali hii? Jaribu kulitumia kundi hili katika shughuli za uinjilisti. Wanafunzi wa vyuoni

wanapenda sana kuulizwa na kushirkishwa kimawazo. Wasikilize na wapatie

Nafasi ya kutoa maoni yao na mapendekezo. Wanajua kile kinachoendelea na wanaweza kushiriki katika kuwafikia wengine.

  5. Vijana Wakubwa – hili kundi mara nyingi hupuuziwa na halitumiwi. Kwa ujumla hawa wanaumri wa watu waliomaliza vyuo; wanatafuta kazi ya kufanya, na wanajaribu kutulia katika jamii na katika kanisa pia. Wanapenda wapewe majukumu na nafasi za uongozi kanisani lakini hawajui waanzie wapi. Kama kanisa likiwatia moyo na kuwatambua itasidia kuonyesha umuhimu wao katika kanisa. Watalifanya kanisa lako likue na liwe moto moto.

  6. Vifaa vya kanisa – Ni vizuri kulichunguza jengo la kanisa kila mwaka. Kila kinachohitajika kurekebishwa na kirekebishwe: Kapeti, rangi, maliwato, vyoo, n.k. Je, kuna mambo makubwa yanayohitaji kujadiliwa? Ikiwa ndivyo bajeti yake itakua je? 7.

  Kalenda kuu ya kanisa – hii inalisaidia kanisa kuona matukio makuu ya mwaka. Itasaidia pia, maidara kujipanga kuunga mkono shughuli mbalimbali za kanisani na kijamii pia.

  8. Misisitizo mikuu – Jaambo gani hasa umgependa ulisisitize katika kwaka – uwakili, michango ya ujenzi, au mikutano ya injili? Nani ataongoza kamati hizi? Je, matukio haya yameingizwa kwenye kalenda kuu ya mwaka? Kumbuka matukio makuu mawili hayawezi kugongana kwa siku moja hiyo hiyo. Hii inaweza kufanya mambo yasifanikiwe au yafanyike kwa viwango dhaifu sana.

  Kuongoza Huduma za Kiibada bada ni jambo muhimu sana katika maisha ya kanisa lolote. Ili ibada imtukuze Mungu, lazima kufikiri

vizuri na kupangilia jambo hio kwa ustadi mkubwa. Hii haina maana kwamba Mzee wa kanisa apangilie kila

kitu mwenyewe, lakini anapaswa kuwasaidia wale ambao wanahusika katika kupangilia huduma za ibada.

Kama Mzee ni jambo la msingi sana kuelewa umuhimu wa ibada kanisani: jinsi inavyotakiwa kumwelekea

Mungu na si mtu, jinsi ibada za namna mbalimbali zinavyo kidhi mahitaji mbalimbali ya wahudhuriaji. Ibada

nyingi zinaelekezwa kwa wale ambao wanaweza kusikia na kutoa mwitikio wao. Je, ibada yako inamvuto

kwa wale wanaopokeaa kwa kutazama na hata kwa wapitaji? Je, mambo gani yanahitajika unapomwabudu

Mungu na unadhani kuna linalohitaji kuboreshwa au kubadilishwa? Ni nani anaiongoza ibada? Je, kushiki

kwa waumini kuko vipi kanisani? Maswali haya yanaweza kujadiliwa na wazee wa kanisa, baraza la kanisa

na hata kamati ya ibada kanisani?

  9 | N o r t h E a s t T a n z a n i a C o n f e r e n c e

  Kutembelea Moja kati ya majukumu ya Mzee wa kanisa kibiblia, ni kujenga mahusiano na watu wa kanisani na jamii kwa ujumla. Hili si jambo linaloweza kufikiwa kwa mtu kuongea na washiriki kila siku ya sabato kwenye shule ya sabato au kusalimiana nje tu ya jingo la kanisa. Utembeleaji ni jambo linaloonekana kufifia. Wazee wanaweza kuwa mfano kwa kuweka mfano wa kutembelea watu. Shirikiana na mchungaji na viongozi wengine kuweka mpango wa matembezi utakao saidia kufanikisha shughuli hii. Washirikishe washiriki pamoja na mashemasi. Hakikisha washiriki na wasio washirki wote mametembelewa Ikiwa kuna watu ambao wamehitaji kujifunza Biblia, je, kanisa linawatembelea watu hawa? Wanaweza kupoa na kupotea ikiwa kanisa halitajali kabisa.

  Tumia mida huu kujenga urafiki na kutambua mahitaji yao ya kiroho. Unapowatembelea watie moyo, na uwaunge mkono. Usiruhusu muda wote utumike kwa kujadili jambo flani ambalo ahaliko sawa kanisani, kumjadili mchungaji au kiongozi flani. Fanya jambo hili kuwa jema na fupi. Ikiwa inadhani kuna haja ya kumtembelea mtu kwa muda mrefu, weka mpango ili ajiandae na umjulishe mapema kabisa.

  Mambo ya kuzingatia kwa mahubiri Ukiwa mzee wa kanisa, tarajia kwamba mara kadhaa utaombwa kutoa huduma ya mahubiri sana. Ikiwa unadhani unahitaji msaada juu ya hili, muone mchungaji wako na ikiwezekana akupatie kozi ndogo ya jinsi ya kuandaa mahubiri. Tumia muda wako wa maandalizi katika maombi, ukimwomba Mungu akusaidie kuupata ujumbe. Hii sio ajenda yako, ni ajenda ya Mungu kutaka kukutumia ili uwalete wengine kwa Yesu. Lipitie hubiri lako kabla ya sabato asubuhi. Jinsi unavyotumia muda wa kutosha kufanya marudio, ndivyo utakavyojiona umekua tayari. Hii itakusaidia kulitoa somo lako kwa kujiamini na kwa usahihi Zaidi.

  Kumbuka kwamba kuhubiri sio tu kusimama na kusoma kifungu cha maneno kwenye kitabu. Tafuta namna ya kuwahusisha watu unaozungumza nao. Tumia vielelezo; chagua jambo moja la kuzungumzia na andaa pointi zako zinazoelekea kwenye kwenye ujumbe uliouchagua. Somo lako liendane na hitaji la kanisa. Hii si nafasi ya kumkemea mtu hadharani, ila ni wakati wa kuwaeleza watu kumgeukia Mungu na kuwakumbusha wajibu wao kwa Mungu.

10 Pr. Almodad Amos

  Semina Fupi kwa Mzee wa kanisa

Kwa sababu ya ratiba ngumu za siku hizi, wakati mwingine ni vizuri kutumia hata

simu zetu. Jambo hili lisitumike kuwa mbadala wa matembezi ya nyumbani,

inaruhusiwa kulifanya hili mara kadhaa ukiwa nyumbani. Hapa kuna mambo

machache unayoweza kufanya kwa kupitia simu:

  

1. Piga simu . Kijatambulishe vizuri na mjulishe kwamba wwe ni Mzee wa kanisa.

  Waambie kwamba wazee wanawapigia washiriki wote simu ili kuwajulia hali na maendeleo yao kiroho.

  Onyesha urafiki 2. . Onyesha kuwajali na kuzijali familia zao.

  3. Zungumza mambo mazuri . Zungumziamambo mazuri yanayotokea kanisani na waulize jinsi Mungu anavyowabariki

  4. Mambo Binafsi . Ikiwa mazungumzo yataelekea kwa mshiriki kumlaumu mshiriki mwingine, mshauri kwanza aende akamuone mshiriki huyo, kwa mujibu wa Mathayo 18:15-17.

  

5. Kushughulika na maombi (Matakwa ya mtu ). Ikiwa mtu ataomba jambo flani

lifanyike, mwambie kuwa utalifuatilia na kurejesah majibu kwake haraka iwezekanavyo. Hakikisha unawarejeshea majibu haraka iwezekanavyo.

  Kumbuka kuwa msiri mara zote

6. . Ikiwa mshiriki amekueleza jambo lake la siri,

usisahau kwamba umefungwa na kukuamini kwake kutokumweleza mtu mwingine yeyote juu ya jambo hilo. Ikiwa unadhani kwamba ni jambo linalohitaji utaratibu wa sharia za kikanisa, wasiliana na mchungaji wako ili akueleze jambo la kufanya

  

7. Hakikisha unapatikana . Wafahamishe kwamba unaweza kuwatembelea muda

wowote ule nyumbani. Wapatie namba yako ya simu. Maongezi yako yawe mafupi na hakikisha unamuombea yule uliyempigia simu.

  N o r t h E a s t T a n z a n i a C o n f e r e n c e 11 | Kuwaandaa Washiriki Kuwa Viongozi Kuwaanda waashiriki kuwa viongozi wa baadae ni moja kati ya majukumu ya Mzee. Hii inahusika na kuwaimarisha kiroho, kuwaleta watu kwa Yesu na kuwafundisha kuzitumia karama zao za roho kwa ajili ya kutoa huduma mbalimbai kanisani. Wasaidie washiki kuzitambua karama zao za roho na wasaidie

kujua wapi na jinsi gani karama zao zinaweza kutumika ktk huduma. Msaidie kila mshirki kujifunza

Zaidi juu ya hizi karama za roho na uwatie moyo kufahamu namna bora ya kuzitumia katika utumishi

wao. Wapatie nafasi ya kutumika kama viongozi katika nafasi mbalimbali ili kanisa itambue kuwa

lnaweza kuwa na viongozi wanaohitajika kabisa.

  

Inashauriwa kwamba viongozi wa kike wawafunze viongozi wa kike huku wale wa kiume wakifunzwa

na viongozi wa kiume. Nafasi ya Mzeee wa kanisa iheshimikena yasiwepo matendo yoyote yale

yanayoonyesha matumizi mabaya ya nafasi hiyo au ulegevu wa namna yoyote katika kazi hii. Kunawakati utahitajika kutoa ushauri kwa mshirki wa kanisa mwenye jinsia tofauti. Kudumisha uadilifu wako wakati wa kutoa ushauri ni jambo la muhimu sana. Viongozi hawapangi kabisa kuanguka katika mitego ya yule mwovu lakini mara nyingi inatokea kuliko tunavyodhani. Tabia ya uasherati ni dhambi ambayo inaweza

kukuharibu wewe, familia yako na kanisa lako pia. Tumia mwongozo huu ili kujepusha na

hatari, na uwe mwangalifu kuchunguza mahali tatitzo lipoelekea. Usiruhusu aina yoyote ile ya

tetesi kuvuma kanisani mwako na katika jamii yako.

  Mambo ya kuzingatia wakati wa kutoa ushauri: 1.

   Usijiweke mwenyewe katika hali ambayo watu hawatakuelewa vizuri. Ikiwezekana wanaume wapate ushauri kutoka kwa wazee wa kanisa na wanawke wapate ushauri kutoka kwa mashemasi wa kike.

  2. Usimshauri mtu mkiwa wawili peke yenu. Uwe na mtu flani karibu (Huyu anaweza kuwa ni kiongozi wako mkubwa wa kanisa au mwenzi wako – mjulishe mtu aliye karibu na wewe kuwa mazungumzo hayo ni ya siri ya hali ya juu sana.) au muwe katika mazingira ambayo ni wazi na watu wanawaona waziwazi.

  

3. Ushauri wenu huu uwakutanishe mara moja au mara mbili, isizidi muda wa saa moja. Ikiwa muda huu

hautawatosha mwelekeze aende kwa mchungaji wake au kwa mtaalamu wa ushauri.

  4. Hakikisa mahusiano yako na Mungu wako yanakua kila siku. Huwezi kuisikia saiti ya Mungu ikiwa hutaki kuzungumza naye.

  5. Angalia viashiria vifuatavyo, ikiwa vinajitokeza, simamisha mazungumzo yenu na muelekeze kwa mtu mwingine. Uko hatarini na unamuweka mtu hatarini ikiwa utajibu maswali yafuatayo kwa kuonyesha ukubali wako: o o Natzamia tutaendelea na mazungumzo haya? Usijali lakini jinsi nilivyovaa.

  

Narekebisha ratiba yangu, angalau nipate muda wa kuonana na wewe tu. Sawa?

Hata awe ni mojakati ya viongozi wa kansia kuwa makini naye sana, jihoji:

12 Pr. Almodad Amos

  Semina Fupi kwa Mzee wa kanisa mchana? Je, nimeanza kumpenda na kuvutiwa na huyu mtu?

   Je, nimeanza kumficha huyu mwenzi wangu baadhi ya mambo ninayofanya pamoja au

   ninayoshauriana na huyo mtu? Je, nadhani siwezi kupoteza uaminifu wangu kwake?

  

Uasherati ni dhambi. Kama kiongozi unaomvuto kwa awtu na watu wanakutazama jinsi

unavyoenenda matendo yako yataathiri watu flani katika umilele wao. Kuchagua kuwa msafi

wa tabia inaaksi usafi wa tabia ya Mungu wako.

  Jinsi ya kumsaidia mchungaji kufanikiwa Mahusiano ya Mzee na Mchungaji 1.

  Kama Mzee, utafanya kazi yako karibu sana na Iombee familia yake kila siku.

  2. mchungaji. Wakati mchungaji ni mwanadamu, Uwe na urafiki na mchungaji wako kwa Zaidi kumbuka ametumwa na Mungu. Mchungaji ya shughuli za kikanisa. hakuja kanisani kwako kwa mapenzi yake 3. Muunge mkono hadharani. Kasha jadilini mwenyewe, lakini kwa kuchaguli na kutiwa tofauti zenu faraghani. mafuta na Mungu kupitia mpango uliowekwa na Konferensi. Mzee anawajibika kuiunga 4. Hakikisha mchungaji wako anapumzika. mkono ofisi ya mchungaji (Hesabu 12:1-10; Ebr Hakuna mtu anayeweza kufanya vizuri ikiwa 13:7, 17). hana muda wa mapumziko.

  5. Muombee mchungaji na familia yake kila siku, Tambua karama za mchungaji wako na jazia na wajulishe kuwa unawaombea. Hili litakua yale ambayo ni mapungufu yake. jambo la kutia moyo sana. Huwezi kujua mzigo 6. Kumbuka hakuna anayeweza kufanya kila kitu. walionao ambao hawawezi kumwambia mtu Mwili wa Kristo unafanya kazi kwa kila kiungo mwingine. Tambua kwamba mchungaji anajua kushiriki kikamilifu. mambo mengi ya siri yanayoendelea katika maisha ya washiriki wake; huu ni mzigo mzito akiubeba peke yake. Ikiwa ulikua hujaanza kufanya hivyo, sasa na uanze

  

Weka na jenga mahusiano ambayo ni Zaidi ya salamu za jumamosi asubuhi

tu. Tambua mambo ambayo mchungaji wako anayapenda. Tafuta namna

mnavyoweza kuzifanya familia zenu ziunganike katika mambo ya kijamii.

Mnapokutana katika mambo ya kijamii, achaneni na mambo ya shughuli za

kanisa, vinginevyo itawazuia kufahamina kwa kuwa mnamambo mengine ya

kikanisa yatakayowafanya msifahamiane.

Usimpinge na kumdhalilisha mchungaji wako hadharani. Ikiwa kunatofauti,

nenda naye faragha na uzungumze kile ambacho ni maoni yako. Kukosoana

hadharani kwa viongozi, kunaleta mpasuko kwa washiriki na huleta hisia

mbaya. Ikiwa waumini watakuletea tetesi juu ya mchungaji, usikubali kabisa.

Ikiwa wanamambo ya kukosoa juu ya mambo ambayo si ya-kikanuni waeleze

kwamba unamuunga mkono mchungaji. Wakumbushe kuwa ikiwa

wanadhani mchungaji amekosea kuna kanuni ya kibiblia ya Mathayo 18 ya

kutatuta tatizo lao. Waulize kama wameifuata kanuni hii na kama sivyo, basi

watie moyo kuifuata

Hakikisha mchungaji wako anamuda na familia yake. Ni jambo rahisi sana

kwa mchungaji kuiacha familia yake kwa sababu ya kazi za ufalme.

  

Elewa kwamba mchungaji naye ni mwanadamu na hawezi kufanya kila kitu

mwenyewe. Ndiyo maana viongozi wengine huchaguliwa ili wasaidie katika

kazi za kanisa. Muunge mkono na uwe tayari kufanya naye kazi. Hitimisho

Ihusishe familia yako na ikuunge mkono katika kazi ya uzee wa

kanisa. Jadilini jinsi jambo hili litakavyoiathiri familia yenu.

Muombeni Mungu awaongoze katika kazi hii na mjukumu haya

mappyapia tambua kwamba wakati mwingine familia yako

iaweza kushambuliwa. Kuna vita isiyoonekana lakini inaendelea,

ingependa kuharibu na kuondoa kabisa huduma yako kwa

kanisa. Wewe na familia yako mnaweza tu kuwa washindi kwa

kuwa na maombi mengi na ibada za mara kwa mara na familia

yako.

  Maelezo ya Huduma ya Mzee wa Kanisa katika Kanisa Mahalia Utangulizi

  Mungu analitaka kanisa kuwa jamii ya watu wenye kusudi moja, ushirika, kukua wakati wote katika Imani na kumjua Yesu Kristo Mwana wa Mungu. Paulo analielezea kanisa kama “. . . mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote ” (Waefeso 1:22). Mungu anatuita katika mwili wake kwa kusudi la kuimarisha uhusiano kwa ajili ya kazi ya wokovu pamoja naye, na katika jamii kila mmoja kushughulikia wokovu wa mwenzake. Roho Mtakatifu huthibitisha fikra zetu, hutuongoza katika toba na kutusimamisha katika kanisa. Ishara ya ubatizo wa maji inaashiria kuingia kwetu katika mwili wa Kristo na pia huashiria uzoefu wa ubatizo wa Roho Mtakatifu kwa huyu mshiriki mpya . “Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.

  ” (Yohana 3:5). Roho Mtakatifu ndiye ambaye ni siri ya uhai wa kanisa. Unapokuja kwa Kristo ni kwa sababu umeandaliwa na Roho Mtakatifu, whoambaye amekuongoza ktk toba ili uwe tayari kwa utumishi (huduma).

  Kanisa linapouhudumia ulimwengu ni namna ya kuonyesha upendo wa Kristo kwa Ulimwengu huu. Ni kanisa linalotakiwa kuyafikia mahitaji ya jamii na kutumiwa na Roho Mtakatifu kama wakala wa wokovu. Kwa hiyo, kanisa ni kiungo kitumishi. Humtumikia Kristo kwa Kumsifu, na kumtumikia kwa kumuhudumia muumini, na pia huutumikia ulimwengu kwa unyenyekevu. “Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo

  ” (Waefeso 2:10). Mungu anamuita kila mshiriki katika utoaji wa huduma ya namna flani. Kanisa ni ufalme wa kikuhani uliowekwa kutoa huduma. Ukuhani wetu ni kuhudumuana kila mmoja na kuuhudumia ulimwengu pia huko nje. Mzee wa kanisa, kama kiongozi mwingine wakanisa, ni mtumishi wa Mungu anayehudumu hekaluni mwake, amepewa karama hiyo na Roho wa Mungu na amepewa agizo la utume kwa ubatizo wa Roho Mtakatifu, (Waefeso 4:11-12). Kazi za Mzee wa Kanisa

Utumishi ambao mtu anaitwa kuufanya pale anapochaguliwa kuwa Mzee wa kanisa, unaweza

kuelezwa kwa namna ifuatayo:

  

1. Kutembelea. Malezi yanalifanya kanisa likue, hasa washiriki wanapotiana moyo mmoja kwa

mwingine. Katika jamii kama hiyo inayojali, hata Mzee wa kanisa anapewa huduma hiyo. Mzee

wakanisa anaweza kuwa mtu wa muhimu sana katika kanisa kama hilo. Mzee awatembelee watu

majumbani mwao, awatie moyo watu wengine kufanya hivyo, na awasasidie pia hata wale ambao si

washiriki kujifunza kushiriki katika huduma hiyo. (Angaalia makundi ambayo hayana familia nayo

pia uayatembelee mahali yalipo).

  

2. Utume wa kanisa. Ni jambo la muhimu sana kwa Mzee wa kanisa kujikita katika utume wa

kanisa na uinjilisti. Washiriki wanataka kujua kama Mzee wao wa kanisa anautambua utume wa

kanisa na kuona akishiriki kikamilifu kabisa. Inasemekana kwamba kanisa linakua kwa waumini

kuiga mfano badala ya kufundishwa tu. Ikiwa Mzee wa kanisa atatenga muda wake kwa ajili ya

shughuli ya uinjiliasti, watu wengine watarithi tabia hiyo na watajiweka wakfu na makini kwa ajili

ya utume wa kanisa. Mzee anatakiwa aweke muda kwa ajili ya kazi ya uinjilisti. Mzee wa kanisa

anakazi ya kusimamia kazi ya kutimiza utume wa kanisa

  

3. Kuongoza Ibada. Jinsi Mzee anavyoongoza ibada za kila juma ni jambo ambalo linaweza kuleta

mabadiliko makubwa sana katika kanisa la Mungu. Uongozi bora katika ibada unaweza kulifanya

kanisa lililopoa, au ibada isiyokua na uhai kuwa ibada yenye maana na iliyo na uhai katika

kumtukuza Mungu. Ujuzi wa kuongoza ibada, kusoma mafungu, maombi ya hadhara, kupangilia

matiririko wa ibada na jinsi ya kufanya mahubiri, ni mambo ambayo Mzee anatakiwa kujifunza.

  

4. Mwalimu wa mambo ya kiroho. Maisha ya kiroho ya mzee wa kanisa marazote yanatakiwa

kuwaongoza washiriki wa kanisa kuutafuta uzoefu wa kina kabisa katika maisha isha yao binafsi ya

kiroho. I Timotheo, sura ya 3, anaelezea maisha ya kiroho ya Mzee wa kania kwa namna ifuatayo:

“. . . mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu,

mkaribishaji, ajuaye kufundisha, si mtu wa kuzoelea ulevi, si mpiga watu; bali awe mpole; si mtu

wa kujadiliana, wala asiwe mwenye kupenda fedha . . .” Mzee atengeneze maisha yake ya kiroho,

kwa kuwa na muda wa faragha wa ibada na mambo binafsi ya kiroho, (jambo hili ni muhimu kwa

kila mkristo anayehitaji kukua kiroho). Mzee ni sharti aaksi tunda la roho kwa kila mtu

atakayehusiana na naye: upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, ukarimu, uaminifu, upole na

kuwa na kiasi.

  

5. Kiongozi na Mtawala katika kanisa. Kama Mzee ni lazima ujitahiti kuweka mchango wa

jambo flani zuri kwa kanisa na maendeleo yake. Kwa kufanya hili, usijaribu kutaka kulipeleka

kanisa kulingana na matakwa yako (domination) bali waruhusu na watu wengine kutoa mawazo yao

katika kanisa na katika huduma. Mzee wa kanisa mara nyingi atashiriki kushauri maidara mengine,

kamati mbalimbali na hata mipango pia. Katika hili, Mzee atalifanya kanisa liwe na umoja katika

kazi zake, atawasilisha mipango kwa baraza, na ataliunganisha kanisa kuufikia utume kwa pamoja.