SEMINA WATENDAKAZI (MAOFISA) WA KANISA
KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO - KONFERENSI YA
MASHARIKI MWA TANZANIA
Miongoni mwa sifa za Uadilifu na za Kidini za Maofisa wa Kanisa ni:
Walio na uwezo Wenye kumcha Mungu Watu wa kweli / si wenye ndimi mbili Wenye kuchukia mapato ya udhalimu Wenye kujawa Roho wa Mungu Wenye kujali na kutunza familia zao / mahusiano mema katika familia Wenye kushuhudiwa mema na watu walio nje Watu wasiolaumika
Wenye kiasi na busara/hekima
Wenye kujali/kufuata utaratibu
Si watu wa kujadiliana(:: si watu
wa kubishana) Wasiwe wepesi wa hasira Wasiwe watu wa kujipendekeza
nafsi zao Walio kielelezo kwa maneno mema na matendo mema, usafi, imani, na upendo.{Kut.18:21; Mdo.6:3; 1Tim.3:1-13; 4:12-16; Tito 1:5-11; 2:1, 7, 8}
(::: Mwangalizi wa Kanisa) Ni daraja lenye madaraka makubwa.
MZEE WA KANISA
- Mzee wa Kanisa Apaswa awe:
1. Aliyejitoa kikamilifu kwa Kristo . “Huwezi kuwa na mvuto
a. Unga mkono mafundisho ya kanisa (Tito 2:1) b. Dumisha mahusiano imara ya familia (1Tim.3:4, 5).
Kama mzee wa kanisa, wewe ni sehemu ya familia mbili; familia yako mwenyewe na familia ya kanisa.
c. Uwe msafi kingono (Ebr.13:4).
Epuka kuvunja miiko ya ngono kwa: 1)
Kumpenda mwenzi wako kama nafsi yako
2. Kielelezo kwa washiriki : Wazee wa kanisa hawana budi kuwa kile wanachotaka wengine kuwa, kuamini kile wanachotarajia washiriki wao kukiamini, na kumpenda Kristo kama wanavyowataka kupenda. Wazee wanachaguliwa na kuwekewa mikono katika kanisa si kwa ajili ya kufanya kazi ya kanisa tu, bali kudhihirisha tabia ya Kristo.
utakaowabadilisha wengine mpaka moyo wako mwenyewe umenyenyekezwa na kusafishwa na kulainishwa na neema ya Kristo” (Evangelism, 458).
Kuwa kielelezo sahihi kwa hakika kutajumuisha yafuatayo:
3) Kuwa na tahadhari unapomshauri mtu wa jinsia tofauti
4) Kuwa imara kiroho
5) Mit.6:32, 33; Thes.4:3-7 iwe kinga yako.
e. Uwe mrudishaji zaka na mtoaji sadaka kielelezo. Ukiwa kielelezo katika hili, unaweza kufanya vingi kuwatia moyo washiriki wa kanisa kuwa mawakili waaminifu.3
3. Kiongozi wa washiriki : Rum.12:8. “Karama ya uongozi ni uwezo wa kutoa
mwelekeo na mwongozo kwa watu wa Mungu ili watende kazi pamoja kutimiza kile Mungu wanachotaka watimize”(MwM,49).
Wapende washiriki wako. Kama ukiwapenda wale unaowaongoza,wengi pia watakupenda. Na kama wanakupenda watafuata uongozi wako.
Unganisha washiriki wako. Kuwasaidia washiriki kuvuta pamoja kwa umoja ni moja ya sehemu muhimu sana za uongozi wa mzee.
Soma Zab.133:1.
Shauriana na washiriki wako. Lisaidie kanisa lako kupanga
malengo yake lenyewe. Panga na wale unaowaongoza na si kwa ajili yao tu.4. Mwezeshaji wa washiriki : Kama mzee, unapaswa uwe mratibu na
mwezeshaji ukitumia mvuto wako kumsaidia kila mshiriki wa kanisa lako
kukuza uwezo kamili wa karama zao binafsi za kiroho kwa ajili ya ujenzi wa
kanisa. >wasaidie washiriki kuzijua karama zao za kiroho, kisha wape mafunzo.2) Kuelewa udhaifu wako
d. Epuka ubaguzi wa aina yo yote (Gal.3:28).
- Baadhi ya Majukumu ya Mzee wa Kanisa:
4. Kuhimiza uwakili katika nyanja zote::: mwili, wakati,talanta, mali, mvuto,
5. Kusimamia ibada za kanisa. kuhakikisha kuwa ibada za kanisa
(Jumatano, Ijumaa, Sabato) ; zinaendesha inavyostahili, na wahudumu
wanaostahili.6. Kuwaandaa wanaotajiwa kubatizwa . Wale wanaohitaji kujiunga na kanisa wanapaswa kujua kanuni zinazoongoza kanisa hilo; wanapaswa kujua maana ya kutoa maisha yao kwa Kristo.
7. Kuwashikiria washiriki wapya . Yapo mambo manne uwezayo kufanya:
a.Wafanye rafiki . Chagua watu miongoni mwa waumini wazoefu ambao watakabidhiwa jukumu la kuwa walezi wa kiroho wa waumini hawa (wajibu wa walezi-MwM, 143)
3. Kuhimiza uinjilisti katika nyanja zote, kupitia idara zote na vyama vyote kanisani.
2. Kulilinda kanisa kwa kutoruhusu mafundisho potovu kuingizwa kanisani.
1. Kulilisha kanisa kupitia mafundisho na mahubiri kanisani na nyumbani mwa washiriki (Mdo.20:28; 1Pet.5:2; Yn.21:15-17). b. Wafundishe .
Endelea kufundisha baada ya ubatizo (Mt.28:20). Wasidie kugundua karama za Roho walizo nazo. Waelimishe jinsi ya kutumia karama hizo kwa busara kuwabariki wengine.
Wasaidie wadumishe mazoea ya kupenda madarasa ya Shule ya Sabato c. Watembelee . Waumini wapya wanapaswa kutembelewa mara kwa mara ili kutiwa moyo katika ukuaji wao kiroho. Waalike nyumbani mwako.
d. Wahusishe .
Washirikishe katika shughuli/programu za kanisa; mfano: huduma za Shule ya Sabato, vijana, uimbaji, kujifunza Biblia, kushuhudia, n.k. Waelekeze namna ya kuongoa roho, wakianza na familia zao na marafiki.
8. Kuwarudisha washiriki waliopotea. Ziko sababu zinazofanya washiriki kupoa
kiroho/kurudi nyuma/kupotea; taz. MwM, 136. Ili kuwarejesha; kwanzawatambue, kisha watembelee. Hapa ni mashauri saba kuongoza safari yako:
i. Uliza maswali kwa busara. ii. Sikiliza kwa makini tena kwa maombi majibu wanayoyatoa. iii. Usilalie upande wo wote katika maongezi yako. iv. Heshimu usiri. v. Waombee. vi. Waalike warejee kanisani. vii. Uwapende.9. Kuwatembelea washiriki nyumbani. Utembeleaji wa washiriki ni muhimu sana kwa malezi na ukuaji wao wa kiroho. Utaratibu wa kutembelea uzingatiwe:
1) Andaa. Andaa moyo wako, ukimwomba Mungu akusaidie kusema na kufanya kile ambacho kitaleta Baraka kwa kila kaya/familia. 2) Fanya urafiki. Unapofika kwenye nyumba husika, anza kuzungumzia mambo ya kawaida ya kijamii yanayojenga. 3) Soma. Baada ya dakika kadhaa, elekeza maongezi yako katika mambo ya kiroho. ….
4) Uliza. Uliza kama lipo jambo fulani au mtu fulani la/wa kuombea. ….
5) Maombi. Waalike watoto na wengine walioko nje wajiunge nanyi.- – ombea maswala waliyokueleza kuwa ndiyo mahitaji yao;
- – mwombee kila mmoja kwa jina lake; - ombea pia asiye muumini anayeishi katika kaya/familia.
6) Ondoka. Ondoka haraka wakati bado utukufu wa ombi unaendelea
kutawala akili za uliowaombea. Katika tamaduni nyingi, nusu saa ni muda wa kutosha katika kutembelea. 7) Andika.- Mara uwapo mbali na nyumba hiyo, yaandike majina ya watu wa nyumba hiyo, iwapo hukuwa nayo.
- Andika mahitaji ya familia hiyo na mapendekezo yao.
- Utakapowatembelea familia hiyo, na kutaja kwa ufasaha mambo
10.Kutoa ushauri kwa mtu mmoja mmoja. Kiongozi anayejali hushauri
na kufariji. Mwongozo wa kushauri: i. Jifunze kusikiliza kwa makini. ii. Jali ufumbuzi. Usitumie muda mwingi kujadili tatizo, bali jadili zaidi ufumbuzi wa tatizo. iii. Wasaidie wachague mpango. iv. Omba pamoja nao. v. Fahamu wakati unapokupasa kutoa rufaa.11.Kuwaunga mkono viongozi wenzake.
Mzee, ni mshauri wa idara zote kanisani. Mzee, anapaswa kufahamu mpango wa kila idara.
Mzee, apaswa kubuni mbinu za kusaidia idara na vyama
kanisani….12.Kusimamia vikao vya kanisa (Baraza la Kanisa / Mashauri ya Kanisa), kwa kushauriana na Mchungaji wa Kanisa / Mtaa (Knn, 2005, 8-23, 25).
13.Kupokea barua na maelekezo toka ngazi za juu za kanisa na kufikisha ujumbe panapohusika.
14.Kutunza siri za washiriki na za vikao vya kanisa.
15.Kupanga/kuratibu huduma maalumu: Ubatizo (MwM, 205-209).
Meza ya Bwana (MwM, 217-223) {Sabato ya 12 ya kila robo. Knn, 2005, 8-15}. Kubariki watoto (MwM, 209-214). Uzinduzi wa kiwanja (MwM, 223-226). Kutenga kundi kuwa kanisa. Kuweka wakfu kanisa/jengo (MwM, 214-217). Mazishi (MwM, 229-232). Maombi kwa wagonjwa (MwM, 239-242). Kuweka wakfu nyumba (MwM, 226-229).
16.Kupanga ratiba ya wahubiri (kwa kushauriana na Mchungaji) na
kuisimamia. “Mamlaka na Majukumu yao ni mapana mno, lakini hayana
budi kutendwa chini ya mwongozo wa mchungaji na mashauriano na baraza la kanisa” (MwM, 43).
“Mamlaka na kazi ya mzee aliyewekewa mikono yanakomea
katika kanisa lile tu alikochaguliwa” (Knn, 2005, 7-12; Church
Manual, 2010, uk.73).
Kikao cha Baraza la wazee / kikao cha wazee na mchungaji:
Chaweza kukutana mara mbili au moja kwa juma…. Wajumbe ni maofisa wasimamizi (i.e.:wazee wote, mashemasi
wakuu, karani wa kanisa, mhazini, mratibu wa usikivu)….
Miongoni mwa mambo muhimu ya kuangalia: Tathmini ya ibada – lishe, matumizi ya muda, ….
Kuona kwamba kalenda ya matukio inazingatiwa na viongozi wa kila idara na vyama kanisani. Kuona maeneo ya kushauri utendaji wa idara au chama kanisani.
Kuona kama mkakati wa malezi ya washiriki kwa mafundisho/ mahubiri na kutembelea unaenda vyema. Tathmini ifanywe mara moja kila juma. Kuangalia hali ya fedha ya kanisa kulingana na mahitaji ya kanisa. Kushauri idara ya uwakili na maendeleo kubuni njia za kuongeza warudisha zaka na watoaji kwa mpango kanisani. Kupitia/kuandaa agenda za kwenda baraza la kanisa/mashauri ya kanisa. Agenda isiyopitia katika kikao hicho, ikitajwa/ikiletwa, ipangwe kujadiliwa kikao kinachofuata. Agenda toka idara huwasilishwa kwa wazee na maelezo. Kutayarisha ratiba ya wahubiri wa kila robo na kuisimamia.
Kufanya tathmini ya maendeleo ya miradi ya kanisa - uinjilisti,
majengo, ….
Kupitia barua toka ngazi za juu za kanisa na kuzifanyia kazi….
Vitabu muhimu kwa mzee wa kanisa:
i. Biblia – uwe na ratiba ya kuisoma kwa ajili ya kukua kiroho.
ii. Kanuni za Kanisa – kila sura iwe bayana kwa mzee wa kanisa.
iii. Mwongozo wa Mzee – kisomwe kila sura na kueleweka. iv. Vitabu vya Roho ya Unabii….- kwa kadri ya nafasi/uwezo. v. Mwongozo wa kujifunza Biblia (lesson) wa kila robo. vi. Kitabu cha Mafundisho ya Biblia – kwa ajili ya darasa la Ubatizo na la Furaha. vii. Pastor’s and Elder’s Handbook for Youth Ministry.Majukumu ya Mzee wa Zamu wa Kanisa:
1. Kuratibu, kuelekeza huduma zote za ibada na shughuli zote za kidini katika juma.
2. Kusimamia waongoza ibada wote, majukumu yao na programu zao (wa S/ Sabato na ibada kuu).
3. Kupokea, kupanga na kutoa matangazo.
4. Kutathmini huduma zote za ibada na shughuli za kidini na kutoa taarifa katika
mkutano wa mchungaji na wazee unaokutana kila katikati ya juma.5. Kupata msaada kutoka kwa wazee na maofisa wengine wa kanisa kila inapohitajika ili kupata uendeshaji wa shughuli za kichungaji uwe laini.
6. Kuratibu shughuli za idara za kanisa.
7. Kuona kwamba mashemasi wa kiume na wa kiume na mabawabu wanaanza shughuli zao kwa wakati, na mahali pa ibada na mikutano ya kidini ni pasafi na pametayarishwa kwa waabuduo au washiriki wa tukio.
8. Kupokea na kushughulikia maswala ya waumini wa kanisa na ya wageni.
9. Kuwa mbunifu katika kuratibu/kuelekeza huduma za kanisa, hivyo kuwasaidia
waongoza ibada za kanisa.10.Kuhamasisha na kuhimiza matumizi mema ya muda katika huduma na shughuli za kanisa kwa nadharia na matendo.
11.Kupangilia utembeleaji wake wa washiriki katika eneo lake alilopangiwa - akiwa na shemasi au mzee mwingine au mchungaji, au peke yake ikibidi.
12.Kupokea na kushughulikia majukumu mengine yo yote kama atakavyoelekezwa na mchungaji.
13.Kuitisha na kuwa mwenyekiti wa kikao cha mchungaji na wazee, mchungaji
asipokuwepo.14.Kuhudhuria darasa la walimu wa Shule ya Sabato.
15.Kushauriana na wazee wenzake kuona kama kuna agenda ya baraza na kuliitisha ikibidi.
16.Kuhakikisha kuwa kama kuna jukumu lo lote lililoagizwa na baraza la kanisa
kutekelezwa, limefanyika.17.Kuandika maoni, mapendekezo, mafanikio juu ya matukio yaliyojili, na mambo ya kutekeleza katika kitabu cha wazee kwa kumbukumbu na kumsadia mahali pa kuanzia mzee wa zamu baada yake.
18.Kuhakikisha kuwa matoleo yote yalikabidhiwa kwa mhazini kwa utaratibu usio
na mashaka.19.Kuthibitisha ufungaji wa taarifa za wiki/mwezi/robo umefanyika, na zile zinazotumwa konferensi zimetumwa vema na kwa wakati.
20.Kukumbusha kanisa matukio yaliyopo yanayotakiwa kufanyiwa kazi kwa pamoja.
-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
---------------------
NJIA 16 ZA KUONGEZA UTOAJI
{Toka Kitabu cha ‘Uwakili na Mtindo wa Maisha TUM’, uk.66-67} (Mwongozo kwa Wachungaji na Wazee wa kanisa)
1. Anzisha Kamati ya Uwakili/Fedha ya Mwaka Mzima. Ukuaji wa uwakili ni
zaidi ya tukio moja la mwaka. Uwakili ni tendo endelevu linalihitaji mikakati ya kutosha kanisani. Kufundisha kwa vitendo na kuwalisha washiriki mambo ya kiroho ndiyo njia pekee iletayo ufanisi.2. Weka malengo makubwa zaidi. Uwezo wa utoaji wa makanisa mengi ni zaidi kuliko unavyoonekana. Malengo makubwa ndiyo yaletayo matokeo makubwa kuliko yaliyotazamiwa.
3. Rudisha mawasiliano ya Kikristo ya kanisa la awali. Mawasiliano ya makanisa ya awali ya kikristo yalifanywa ana kwa ana, mtu kwa mtu, mkakati katika vikundi vidogo vidogo ndivyo walivyofanikiwa. Lazima tuwatembelee washiriki wote na kuwatia moyo, matokeo yake yatakuwa kama yale ya kanisa la mitume.
4. Toa zaidi kwa utume. Maofisa wa kanisa(wajumbe wa baraza la kanisa) wawe
kielelezo katika utoaji kwa mpango….5. Badilisha mtindo wa kumtembelea kila mshiriki. Badala ya kuanza kufuatilia wasioitikia, wafuatilie kwanza unaowatarajia zaidi kuitika. Tumia 85% ya muda wako mahali unapotegemea 85% ya fedha.
6. Jizatiti. Kuwa mchungaji/mzee wa kanisa unayewezesha wakurugenzi wa
uwakili ; usiwafanyie kazi yao. Usizuie juhudi yao. Usikubali kuwa mwenyekiti
wa kamati yo yote ya uwakili.7. Wapange watoaji wako wazuri. Katika upaliliaji na ukuaji wa uwakili tumia
watoaji wako wazuri wakusaidie kuliambukiza kanisa lote kuwa na tabia ya
kudumu katika utoaji.
8. Fundisha umuhimu wa utoaji. Fundisha, hubiri utoaji kwa mpango. Usikingie
kifua utoaji wa ahadi ati kwa sababu kanisa linahitaji kupanga mipango yake.
Washiriki wanahitaji kufanyia uamuzi juu ya uhusiano wao na Mungu.
9. Watie moyo washiriki juu ya kutoa kwa mpango. Kutoa zaka na sadaka ni
sehemu muhimu ya ibada. Mungu alipanga utoaji wa mpango kwa faida ya
mwanadamu ili aokolewe na doa la uchoyo.10. Watambue na uwaheshimu watoaji waaminifu. Kwa ruhusa ya watoaji wafahamishe wengine mibaraka wanayoipata kama vyombo vyake.
11. Eleza jinsi ya kutoa. Kwa familia nyingi, tutoe kiasi gani ni jambo gumu.
Jitayarishe kutoa maelekezo na vigezo vitakavyosaidia familia fulani na siyo
maelekezo ya jumla.12. Fanya maongezi ya faragha. Ushauri juu y utoaji wa kikristo wapaswa kuwa wa faragha sana na ufanyike nyumbani. Ruhusu jambo hili liwe kati ya mshiriki na mshiriki. Ni vyema wachungaji wasijiingize hapa, mshiriki amsaidie mshiriki.
Fikiria mchungaji mwenye washiriki elfu tatu katika mtaa!
13. Tia moyo utoaji wa ushuhuda binafsi. Njia yenye nguvu na iliyo bora ni ile
ya kutoa ushuhuda kwa wale wenye uzoefu wa injili na matokeo ya utoaji mwema.14. Waachie wahiriki wajivunie (utoaji). Kadri utoaji unavyopanda kuelekea magoli yake, tangaza habari hizi njema. Endelea kutangaza kadri matoleo yamiminikavyo. Tangaza mafanikio sio ushindwaji.
15. Waelimishe na mapatie malengo washiriki wapya mara baada ya
kubatizwa. Waonyeshe kuwa, kuwa mshiriki wa familia ya Mungu na kutoa
ahadi ya ubatizo ni sawa na pande mbili za sarafu moja. Kwamba, kufungamanisha fedha zake na ushirika wa kanisa, hufanya ushirika wake kuwa halisi, bila mashaka.16. Fedha za mipango mikubwa zichangishwe tofauti na zingine. “Kama fedha za ujenzi zingelitafutwa kwanza, tena kwa bidii kubwa, kanisa likaonekana halina madeni – Je mambo yangelikuwa vizuri iliyoje?” CS, uk.259, 260.
VITABU VYA REJEA : o Kanuni za Kanisa, Toleo la 17, 2005. o Mwongozo wa Mzee. o Uwakili ni Mtindo wa Maisha-TUM.
KARANI WA KANISA - wadhifa muhimu.
A. Baadhi ya Majukumu ya Karani wa Kanisa: 1. Huhudumu kama katibu wa baraza la kanisa.
3. Hutunza orodha sahihi ya washiriki wa kanisa:- Kila jina la mshiriki liwe na kumbukumbu za mapokeo –tarehe ya baraza na jinsi alivyoingia: ikiwa ni kwa ubatizo, kuhamia (barua) au kupokelewa kwa mikono.
b) ya kuwasilisha kanisani.
c) Nje ya Konferensi, ndani ya Union au nje ya Union
b) Nje ya mtaa, ndani ya Konferensi;
a) Ndani ya mtaa;
11. Kuzingatia uandishi wa barua za miito:
10. Kutunza siri za washiriki.
9. Kutayarisha bajeti ya ofisi yake ya mwaka.
a) ya kwenda Konferensi,
Kila jina lililoondolewa liwe na kumbukumbu za maondoleo –ikiwa ni kwa barua(kuhama), kuasi, kifo, au kutojulikana aliko.
8. Kuandaa taarifa kila robo;
2. Huhudumu kama katibu wa mikutano yote ya Mashauri ya Kanisa.
6. Kutayarisha na kukabidhi vyeti vya ubatizo, ushirika, kubariki watoto, kwa wahusika kwa wakati.
5. Huandika majina ya wabatizwa katika kitabu cha washiriki mara baada ya ubatizo wao. Kila jina linaloongezwa kwa orodha ya washiriki, liongezwe pia kwa mahudhurio ya Meza ya Bwana.
Majina ya wasio washiriki wa kanisa mahalia hawaorodheshwi katika orodha ya washiriki wa kanisa, wala ya mahudhurio ya Meza ya Bwana.
Orodha ya mahudhurio ya Meza ya Bwana ni sawa na ile ya washiriki wa kanisa (mapokeo).
4. Hutunza orodha sahihi ya mahudhurio ya Meza ya Bwana:-
7. Kutunza orodha ya mali za kanisa.
Karani wa kanisa huandika barua kwa agizo la Baraza la Kanisa, Mkutano wa Mashauri ya Kanisa, au bodi ya wazee wa kanisa.
12. Kuratibu zoezi la kuelimisha washiriki juu ya mshiriki na ushirika.
B. Mipaka ya Karani wa Kanisa:
Asitunze pembeni orodha ya washiriki waliorudi nyuma au wasiojukana walipo.
Asitoe barua kwa mshiriki ye yote aliye chini ya karipio.
Asiongeze jina bila idhini ya Kanisa.
Asiondoe jina bila idhini ya Kanisa, isipokuwa kwa kifo.
REJEA: KANUNI ZA KANISA, Toleo la 17, 2005.
(m.y. mtumishi wa kanisa) {Mdo.6:3-6; 1Tim.3:8-13; Rum.16:1,2} SHEMASI
Wawe kielelezo katika tabia na mwenendo wa Kikristo (wacha Mungu).
Shemasi wa kiume sharti awekewe mikono kabla ya kushika kazi yake.
Shemasi mkuu (me & ke) ni wajumbe wa baraza la kanisa.A.
: Baadhi ya Majukumu ya Shemasi
1. Kusaidia katika Ibada na Mikutano, Kukaribisha wageni na washiriki wanapoingia kanisani.
Kuhakikisha kuwa waabudu wamekaa katika mpango mpango stahili. Kuhakikisha kuwa kuna utulivu mahali pa ibada. Zamu ipangwe vizuri na kufuatiliwa na shemasi mkuu.
2. Kutembelea washiriki nyumbani mwao {malezi} Kufanikisha zoezi hili muhimu sana katika malezi ya washiriki, ni vyema kila shemasi awe na nyumba anazohudumia.
Mpango mzuri na utaratibu wa kuwatembelea washiriki uwepo; Utembeleaji wa washiriki nyumbani mwao ni muhimu sana kwa malezi na ukuaji wao kiroho. Utaratibu wa kutembelea uzingatiwe: 1) Andaa. Andaa moyo wako, ukimwomba Mungu akusaidie kusema na kufanya kile ambacho kitaleta Baraka kwa kila kaya/familia. 2) Fanya urafiki. Unapofika kwenye nyumba husika, anza kuzungumzia mambo ya kawaida ya kijamii yanayojenga. 3) Soma. Baada ya dakika kadhaa, elekeza maongezi yako katika mambo ya kiroho. …. 4) Uliza. Uliza kama lipo jambo fulani au mtu fulani la/wa kuombea. ….
- – ombea maswala waliyokueleza kuwa ndiyo mahitaji yao;
- – mwombee kila mmoja kwa jina lake;
- ombea pia asiye muumini anayeishi katika kaya/familia.
- Mara uwapo mbali na nyumba hiyo, yaandike majina ya watu wa nyumba hiyo, iwapo hukuwa nayo.
- Andika mahitaji ya familia hiyo na mapendekezo yao.
- Utakapowatembelea familia hiyo, na kutaja kwa ufasaha mambo mliyogusia kwenye ziara yako ya awali katika familia hiyo, huishawishi familia hiyo kuamini kuwa kwa hakika unawapenda na kuwajali.
Kutawadhana miguu {ufafanuzi wa namna ya kuhudumia wakati wa jukumu hili} .
REJEA: Kanuni za Kanisa, Toleo la 17, 2005.
Haruhusiwi kusimamia mkutano wa kupokea na kuhamisha washiriki.
Haruhusiwi kuendesha huduma zo zote zile za kanisa zitendwazo na
mchungaji aliyewekewa mikono.12.Wawe mstari wa mbele kuhudhuria ibada za kanisa.
11.Kuandaa bajeti ya mashemasi ya mwaka.
9. Kuendesha huduma ya mazishi (shemasi wa kiume) 10.Kuhudhuria katika bodi ya mashemasi.
Meza ya Bwana {ufafanuzi wa namna ya kuandaa mkate na divai na namna ya kuhudumu} .
8. Kusaidia katika huduma za kanisa: Ubatizo {ufafanuzi wa kuandaa mahali pa ubatizo na kupokea wabatizwa toka majini} .
5) Maombi. Waalike watoto na wengine walioko nje wajiunge nanyi.
7. Kutunza siri za washiriki.
6. Kukusanya zaka na sadaka siku ya ibada, kuzihesabu na kuzirekodi, kisha
kumkabidhi mhazini, naye kuwapatia stakabadhi kwa kiasi alichokabidhiwa.5. Kuwatunza wagonjwa na maskini (mfuko wa wenye shida uwepo).
4. Kuangalia usafi wa jengo la kanisa, vifaa vya kanisa, na uwanja wake.
Kufanya ukarabati inapobidi.
3. Kutunza mali za kanisa,
Kuwe na orodha ya mali za kanisa na kutunzwa mahali stahili.
Taarifa ya kutembelea hutumwa Konferensi kupitia katibu wa uwakili.
6) Ondoka. Ondoka haraka wakati bado utukufu wa ombi unaendelea kutawala akili za uliowaombea. Katika tamaduni nyingi, nusu saa ni muda wa kutosha katika kutembelea. 7) Andika.
B. Baadhi ya mipaka ya shemasi :
- – Kazi Takatifu.
MHAZINI WA KANISA
Mhazini anaweza kwa sehemu kubwa kuchangia moyo wa uaminifu katika
kurudisha zaka na kukuza roho ya ukarimu miongoni mwa washiriki.
Baadhi ya Majukumu ya Mhazini wa Kanisa :-
1. Mwangalizi/Mtunzaji wa fedha zote na kanisa:- a) Fedha za amana – ziendazo Konferensi.
b) Fedha za kanisa mahalia.
c) Fedha za mashirika saidizi ya kanisa mahalia (fedha za idara na vyama kanisani)
2. Kutuma fedha za amana (Trust Funds) kulingana na ratiba ya Konferensi.
Kanisa haliwezi kukopa, kutumia, au kuzuia fedha za amana kwa madhumuni yo yote yale.
3. Kusimamia matumizi ya fedha za kanisa mahalia na za mashirika saidizi kanisani.
Fedha za kanisa mahalia hutumika kwa agizo la baraza la kanisa au mashauri ya kanisa. Fedha za idara na vyama (mashirika saidizi) hutolewa kwa idhini ya mabaraza ya idara/vyama husika. Awe mwangalifu kuona kuwa anapewa stakabadhi kwa malipo yote yaliyofanywa. Taarifa ya marejesho ni muhimu kabla kiongozi wa idara/ofisa hajaomba fedha zingine.
4. Kutoa risti kwa kila pesa anayopokea.
5. Kulinda kusudi la pesa Mhazini wa Kanisa au Baraza la Kanisa hawana mamlaka ya kuchepusha fedha zo zote kutoka kwa lengo ambalo kwalo zimetolewa.
6. Kutayarisha na kutuma taarifa Konferensi kila mwezi.
7. Kutayarisha na kutoa taarifa kwa Baraza la Kanisa na Mkutano wa Mashauri ya Kanisa kila robo.
8. Kujaza Jicho la Kanisa kila mwezi.
9. Kuhesabu na kuandika idadi ya wanaorudisha zaka na wanaotoa kwa mpango
(washiriki na wasio washiriki).
10.Kuelimisha washiriki uzuri wa kutoa zaka na sadaka kwa njia ya bahasha tena
kwa mpango.11.Kuelimisha washiriki wanaorudisha zaka na kutoa sadaka zao kwa njia ya hawala au hundi ya posta, mlipwaji awe ni kanisa, badala ya mtu binafsi ye yote yule. Kisha awasilishe pay in slip kwa mhazini ili amkatie risti.
12.Kuhudhuria Baraza la Kanisa kila mwezi.
13.Kutayarisha bajeti ya ofisi yake kwa mwaka.
14.Kuzingatia utaratibu mzuri wa kutuma fedha Konferensi:- Pamoja na kuandika vizuri jina na A/C ya Konferensi kwenye pay in slip; Jina la Kanisa linalotoa taarifa liandikwe pembeni kushoto mwa pay in
Kuhakikisha muhuri na sahihi ya ‘teller’ wa benki viko sawa.
15.Kutunza siri za washiriki.
REJEA: Kanuni za Kanisa, Toleo la 17, 2005.
MRATIBU WA USIKIVU
Ni muhimu kwamba wengi walio na shauku iliyokuzwa kupitia juhudi za utume wa kanisa wahudumiwe mara moja. Kufikia hapo, mratibu wa usikivu ambaye anaweza awe mzee wa kanisa achaguliwe wakati wa uchaguzi wa maofisa wa kanisa. Mtu huyu ni mjumbe wa baraza la kanisa na wa Kamati ya Huduma za Uinjilisti wa Washiriki, naye hutenda kazi moja kwa moja na mchungaji na mwenyekiti wa kamati hiyo. Majukumu yanayohusika na wadhifa ni pamoja na :-
1. Kutunza orodha sahihi ya wale wote wenye shauku, iliyopokelewa na kanisa kutokana na kila chanzo kama vile Huduma za Jamii (Chama cha Dorkas), Sadaka ya Mavuno, mikutano ya uinjilisti wa hadhara, masomo ya Biblia, uinjilisti wa walei, mawasililiano yatokanayo na kushuhudia, kugawa magazeti, uinjilisti wa Shule ya Sabato, uinjilisti wa vitabu, uinjilisti wa afya na kiasi, radio-televisheni, na vitabu vinavyotolewa na kanisa kwa ajili ya utume.
2. Kumsaidia mchungaji na mwenyekiti wa Huduma za Uinjilisti wa Washiriki katika kuandikisha na kuorodhesha majina ya washiriki wenye sifa kwa ajili ya huduma ya ufuatiliaji.
3. Kutoa taarifa kwa baraza la kanisa kila mwezi juu ya idadi ya wasikivu waliopokelewa na idadi ya wale waliofuatiliwa. Pale ambapo mtu aliyefuatiliwa anapokuwa amefundishwa vya kutosha, basi akabidhiwe kwa mchungaji.
REJEA: Kanuni za Kanisa, Toleo la 17, 2005; Sura 7-31, 32.
KIONGOZI / MKUU WA KUNDI : Baadhi ya majukumu ya Kiongozi (Mkuu) wa Kundi
1. Kiongozi wa kiroho kundini (akimsaidia Mzee wa Kanisa) i. Anapaswa kuwapenda wale anaowaongoza
Mwenye huruma Awe na tamaa ya kuwasaidia wakue kiroho Kuwapenda licha ya kasoro zao ii. Tafuta ushauri wa washiriki kundini na kwa Mzee wa Kanisa
2. Kuwaunga mkono watendakazi wenzake kundini Buni mbinu za kusaidia kila mtendakazi afaulu Washirikishe wanakundi katika mipango ya kundi, na ya Kanisa
3. Kulilisha kundi, mzee wa Kanisa asipokuwepo Awe na uwezo wa kuendesha ibada za Kanisa, kuhubiri na kufundisha Kusimamia huduma ya maombi kundini Kutoa mafundisho na semina kulenga mahitaji ya wanakundi
4. Kuunga mkono / kutetea kanuni za Kanisa na Mafundisho ya Kanisa
5. Kushirikiana na Kanisa na Konferensi Kutekeleza mipango toka Kanisa mahalia na Konferensi Kuwaheshimu viongozi hao na kuwaunga mkono Kuwashauri
6. Kulilinda kundi kwa kutoruhusu mafundisho potovu kuingizwa kundini 7. Kuhimiza uinjilisti katika nyanja zote.
8. Kuhimiza uwakili katika njanja zote, mkuu wa kundi ukiwa kielelezo (Lk.
12:42) Matoleo: Zaka na Sadaka i.e. utoaji kwa mpango Matumizi ya muda, ikiwemo utunzaji wa Sabato na kazi siku sita.
Matumizi ya talanta/karama Kutunza mwili kama hekalu Mvuto
9. Kuwashirikisha vijana wadogo na watoto katika huduma za Kanisa na uinjilisti
Yapo mambo manne uwezayo kufanya: a. Wafanye rafiki. Chagua watu miongoni mwa waumini wazoefu ambao watakabidhiwa jukumu la kuwa walezi wa kiroho wa waumini hawa wapya.
10. Kuwashikiria washiriki wapya.
(wajibu wa walezi-MwM, 143) b. Wafundishe.
Endelea kufundisha baada ya ubatizo (Mt.28:20). Wasidie kugundua karama za Roho walizo nazo. Waelimishe jinsi ya kutumia karama hizo kwa busara kuwabariki wengine.
Wasaidie wadumishe mazoea ya kupenda madarasa ya Shule ya Sabato c. Watembelee. Waumini wapya wanapaswa kutembelewa mara kwa mara ili
kutiwa moyo katika ukuaji wao kiroho.
Waalike nyumbani mwako.d. Wahusishe.
Washirikishe katika shughuli/programu za kanisa; mfano: huduma za Shule ya Sabato, vijana, uimbaji, kujifunza Biblia, kushuhudia, n.k.
Waelekeze namna ya kuongoa roho, wakianza na familia zao na marafiki.
11. Kusimamia kikao cha kundi
12. Kuhudhuria Baraza la Kanisa kila mwezi
13. Kuhimiza uwasilishaji wa taarifa zitokazo kundini kwenda Kanisa mahalia – Mhazini, Katibu wa Uwakili, Huduma za Washiriki, Shule ya Sabato na wengineo.
14. Kusimamia na kutetea kalenda ya matukio ya mwaka na mpango wa Kanisa.
15. Kutembelea waashiriki nyumbani;
Utembeleaji wa washiriki ni muhimu sana kwa malezi na ukuaji wao wa kiroho. Utaratibu wa kutembelea uzingatiwe: 1) Andaa. Andaa moyo wako, ukimwomba Mungu akusaidie kusema na kufanya kile ambacho kitaleta Baraka kwa kila kaya/familia. 2) Fanya urafiki. Unapofika kwenye nyumba husika, anza kuzungumzia mambo ya kawaida ya kijamii yanayojenga. 3) Soma. Baada ya dakika kadhaa, elekeza maongezi yako katika mambo ya kiroho. …. 4) Uliza. Uliza kama lipo jambo fulani au mtu fulani la/wa kuombea. …. 5) Maombi. Waalike watoto na wengine walioko nje wajiunge nanyi.
- – ombea maswala waliyokueleza kuwa ndiyo mahitaji yao;
- – mwombee kila mmoja kwa jina lake; - ombea pia asiye muumini anayeishi katika kaya/familia.
6) Ondoka. Ondoka haraka wakati bado utukufu wa ombi unaendelea kutawala akili za uliowaombea. Katika tamaduni nyingi, nusu saa ni muda wa kutosha katika kutembelea. 7) Andika.
- Mara uwapo mbali na nyumba hiyo, yaandike majina ya watu wa nyumba hiyo, iwapo hukuwa nayo.
- Andika mahitaji ya familia hiyo na mapendekezo yao.
- Utakapowatembelea familia hiyo, na kutaja kwa ufasaha mambo mliyogusia kwenye ziara yako ya awali katika familia hiyo, huishawishi familia hiyo kuamini kuwa kwa hakika unawapenda na kuwajali.
16. Kuliandaa kundi kuwa kanisa.
IDARA KANISANI (ASASI SAIDIZI KANISANI)
A. KWA NINI IDARA KANISANI?
Sababu za Kuwepo Idara Kanisani:
1. Kugawa majukumu
2. Kuongoa roho
3. Kutoa ushauri kwa uongozi wa kanisa
6. Usomaji wa vitabu vya Roho ya Unabii 7. Ushuhudiaji.
Idara ya Huduma za Washiriki hutoa nyenzo na kuwafunza washiriki wa kanisa kuunganisha juhudi zao pamoja na za wachungaji na maofisa wa kanisa katika hitimisho la kutangaza injili ya wokovu katika Kristo. Lengo ni
<><><> Tuma taarifa iendayo Konferensi kwa wakati, kulingana na
utaratibu uliopewa Kiongozi, uwe kielelezo katika usemi, mwenendo, usafi, uwakili wa muda, uaminifu na uadilifu katika nyanja zote.
8) Weka watu wanaofaa katika nafasi wanazostahili. 9) Wafundishe (unaowaongoza) katika lugha yao na kasi yao. 10) Kagua kazi ulizowapa, himiza ufanisi wa kazi; daima watie moyo. 11) Chukua taarifa ya kazi kwa wakati, peleka katika ngazi zinazohusika. 12) Shirikiana na maofisa wenzako. 13) Toa shukrani kwa kazi njema.
14) Kamwe usifanye matumizi ya fedha za idara bila kuidhinishwa na idara husika
kupitia vikao vyake.6) Peleka mipango na mapendekezo kwenye baraza la kanisa. 7) Wape wenzako madaraka, yaani, washirikishe wenzako katika kutekeleza majukumu.
2) Mwombe Mungu akuongoze na akuwezeshe kutekeleza jukumu alilokupa.
3) Uliza mashauri toka kwa watu wengine – mf. Mchungaji, mzee wa kanisa, ….
4) Uwe na mipango/malengo ya muda mfupi na ya muda mrefu.5) Wahusishe wana idara katika mipango/malengo hadi waone kwamba ni yao
wala siyo yako tu.5. Usomaji wa Biblia kwa mpango
4. Kushirikiana idara moja na nyingine kutenda kazi za kanisa
4. Mahudhurio katika ibada za kanisa na mikutano ya kiroho
3. Usomaji wa miongozo hiyo
2. Ununuzi wa miongozo ya kujifunza Biblia
1. Uaminifu katika kurudisha zaka na sadaka
Viwango vya Kiroho Vipasavyo Kuinuliwa na Idara Kupitia Utendaji:
5. Kuinua viwango vya kiroho kanisani
B. NJIA ZA KUENDESHA IDARA KANISANI: 1) Tambua ukubwa wa idara unayoisimamia na changamoto zilizopo.
IDARA YA HUDUMA ZA WASHIRIKI
kuandikisha kila mshiriki katika utendaji wa dhati wa huduma ya Mungu ya uongoaji roho.
A. Baadhi ya majukumu ya Kiongozi wa Hduma za Washiriki:
1. Kuongoza katika kufunza na kuliongoza kanisa katika huduma ya utendaji wa utume.
2. Mwenyekiti wa Baraza la Huduma za Washiriki
3. Kuwasilisha kwa Kanisa, katika hduma ya Sabato ya kila mwezi na mikutano ya mashauri ya kanisa, taarifa kuhusu shughuli kamili za utume wa Kanisa.
B.
Baadhi ya majukumu ya Katibu wa Huduma za Uinjilisti:
1. Kufanya kazi kama Katibu wa Baraza la Huduma za Uinjilisti.2. Kutoa taarifa kwa Kanisa juu ya shughuli za Huduma za Uinjilisti wakati wa huduma ya Sabato ya kila mwezi wa Huduma za Uinjilisti na katika mkutano mashauri ya Kanisa.
3. Kuhusika katika manunuzi yote yanayofanywa na Kanisa katika Duka la Vitabu la Waadventista.
4. Kulifahamisha Kanisa kuhusu nyenzo zinazopatikana kwa ajili ya matumizi yake.
5. Kupanga sadaka za mara kwa mara ili kuwezesha Huduma za Uinjilisti kupata vifaa kwa ajili ya washiriki kufanyia kazi ya utume pale ambapo vifaa hivyo havipatikani kupitia bajeti ya Kanisa. Sadaka ya huduma za Uinjilisti kwa ajili ya kusudi hili inaweza kutolewa katika Sabato ya kwanza ya mwezi.
6. Kuandaa na kuwasilisha kwa wakati taarifa iendayo konferensi kila robo, hali kadhalika ile iendayo mashauri ya Kanisa.
C. Baadhi ya majukumu ya Kiongozi wa Chama cha Wanaume Waadventista (AMO):
1. Kuratibu na kusimamia usajili wa wanachama
2. Kusimamia mikutano ya wanachama ya kila juma
3. Kuongoza wanachama kutekeleza uafuatayo:- Kugawa misaada ya vitu (misaada ya kiutu) magazeti, hospitalini, vituo
- vya kulea watoto yatima, n.k. Kuhudumia Nyumba za wenye shida, wazee wasiojiweza, wakongwe,
- (kuratibu ukaarabati au ujenzi wa Nyumba) Huduma kwa wagonjwa walio majumbani
- Huduma ya uinjilisti magerezani
- Kutoa ushauri
- Kuratibu na kusimamia utoaji wa elimu ya watu wazima pale
- inapohitajika.
D. Baadhi ya majukumu ya Katibu-Mhazini wa Chama cha AMO:
1. Ni mwandishi na mtunza kumbukumbu ya vikao vya chama
2. Ni mtunzaji wa vifaa vya chama
3. Kupokea michango ya wanacham na kuwasilisha fedha kwa Mhazini wa Kanisa. Mhazini wa Kanisa ndiye benki ya chama.
4. Kutoa taarifa ya mapato na matumizi ya fedha za chama kwa wanachama kila mwezi.
E. Baadhi ya majukumu ya Kiongozi wa Chama cha Dorkas:
1. Kuratibu na kusimamia usaji wa wanachama
2. Kusimamia mikutano ya wanachama ya kila juma
3. Kuongoza wanachama kutekeleza yafuatayo:- Kugawa misaada ya vitu (misaada ya kiutu) magerezani, hospitalini, vituo vya kulea watoto yatima, n.k.
Kuhudumia Nyumba za wenye shida (maskini), wazee wasiojiweza, wakongwe (kwa maombi, mavazi, vyakula, n.k. Huduma kwa wagonjwa walio majumbani (kwa maombi, chakula, madawa, n.k.) Huduma ya uinjilisti magerezani Kutoa ushauri nasaha Kushirikiana na chama cha AMO katika utoaji wa elimu ya watu wazima pale inapohitajika.
F.
Baadhi ya majukumu ya Katibu-Mhazini wa chama cha
Dorkas:1. Ni mwandishi na mtunza kumbukumbu ya vikao vya chama
2. Ni mtunzaji wa vifaa vya chama
3. Kupokea michango ya wanachama na kuwasilisha fedha kwa Mhazini wa Kanisa. Mhazini wa Kanisa ndiye benki ya chama
4. Kutoa taarifa ya mapato na matumizi ya fedha za chama kwa wanachama kila mwezi.
G. Baadhi ya majukumu ya Kiongozi wa Satelite:
1. Kuona kwa dishi na vifaa vingine vya Satelite vipo katika hali njema
2. Kupata vipindi vinavyorishwa kwa satellite vifaavyo Kanisa mfano Hope Channel.
3. Kuwa na ratiba ya kuonyesha program za satellite zenye mafunzo / masomo yaffayo kwa Kanisa. Yaweza kurekodiwa na kuonyeshwa kwa washiriki kwa ratiba mwafaka, usingoje tu mikutano ya uinjili kwa njia ya satellite.
4. Pale ambapo Kanisa bado halina satellite, kiongozi huyu ahamasishe na kusimamia ununuzi wa vifaa na matumizi yake, akionyesha faida nono za kuwa na nyezo hii muhimu ya uinjilisti.
5. Kupanga na kusimamia bajeti ya satellite.
H . Baadhi ya majukumu ya Mratibu wa Huduma kwa Watu
:
Wenye Ulemavu
Washiriki la kanisa la palepale litoe uangalifu maalumu kwa washiriki na wengine walio walemavu. Likuze programu ya kushuhudia kwa walemavu; likitoa mapendekezo kwa baraza la kanisa kuhusu hatua zitakazowezekana kuchukuliwa ili kufanya vifaa vya kanisa viweze kupatikana kwa urahisi kwa walemavu; kulisaidia kanisa kutatua matatizo ya usafiri kwa walemavu. Mratibu wa Huduma kwa watu walemavu hutumika kama kiungo kwa
Kupitia kwa Huduma kwa watu walemavu, Baraza la Huduma za
asasi zinazotoa huduma kwa watu walemavu kama vile Shirika la Huduma za Kikristo kwa Wasioona na kukuza programu za shirika hilo kanisani.
REJEA: Kanuni za Kanisa, Toleo la 17, 2005.
IDARA YA SHULE YA SABATO
Shule ya Sabato ndiyo mfumo kimsingi wa elimu ya kidini ya Kanisa la Waadventista Wasabato na una makusudi manne: kujifunza Maandiko Matakatifu, ushirika, kuifikia jamii (kushuhudia), na kukazia utume ulimwenguni.
A. Kazi za Maofisa wa Shule ya Sabato :-
1. Kiongozi (Mrakibu) wa Shule ya Sabato
Anatazamiwa kufuata maamuzi ya Baraza la Shule ya Sabato kuhusu utendaji wa idara.
Baadhi ya majumu yake:
i. Kusimamia viongozi wote wa Shule ya Sabato na kuwatia moyo kutekeleza majukumu yao kwa furaha na mafanikio. ii. Kuitisha na kuwa mwenyekiti wa Baraza la Shule ya Sabato. iii. Kusimamia utekelezaji wa maamuzi ya Baraza la Kanisa katika idara ya Shule Sabato. iv. Kusimamia mkutano wa Walimu wa Shule ya Sabato. v. Kuwakilisha Shule ya Sabato kwenye Baraza la Kanisa. vi. Kuona kwamba migawanyo yote inafanywa sawasawa. vii. Kupanga kutimiza mahitaji ya kila divisheni kwa maofisa, vifaa / zana, na fedha. viii. Kupanga na msaidizi wa Shule ya Sabato – uinjilisti kuhamasisha
VBS, kufanya Matawi ya Shule ya Sabato, na uinjilisti kupitia madarasa ya Shule ya Sabato ix. Kupanga na msaidizi wa Shule ya Sabato – Ushirika kutafuta kurudisha washiriki waliorudi nyuma, kwa kuweka hai rekodi za
Shule ya Sabato na kuwatia moyo viongozi na walimu kupanga program mathubuti za kutembelea x. Kuwasiliana na Karani wa Shule ya Sabato juu ya ukamilifu wa rekodi na usahihi wa taarifa na utumiaji wa hizo taarifa haraka kila robo kwenda kwa Mkurugenzi wa Shule ya Sabato Konferensi kupitia kwa Mchungaji wa Mtaa. xi. Kuhimiza malengo manne ya Shule ya Sabato xii. Kusimamia mpangilio na uundishaji katika migawanyo kama ifuatavyo:-
a. Kupanga na kuratibu mikutano ya walimu wa Shule ya sabato b. Kuwahi kila sabato asubuhi kuratibisha shughuli, kujibu maswali, kusaidia kutafuta wa badala pale ambapo waliopangwa kawakufika
c. Kutoa uongozi na kutia moyo viongozi wa migawanyo
d. Kuwa kiunganishi cha Kanisa na migawanyo mingine kwa kuhimiza matoleo ya Shule ya Sabato ya 13 e. Kuhimiza mahudhurio katika darasa la walimu.
2. Kiongozi Msaidizi wa Shule ya Sabato – Ushirika Baadhi ya majukumu yake:
i. Kutunza orodha ya washiriki wa Shule ya Sabato, anuani na namba zao za simu ii. Kuhimiza utembeleaji wa washiriki wasiohudhuria vyema Shule ya
Sabato iii. Kusaidia kuhusishwa kwa wabatizwa wapya na wahamiaji katika programu za Shule ya Sabato iv. Kuhudhuria baraza la Shule ya sabato na kutoa taarifa juu ya shughuli na mipango kwa ajili ya kukuza ushirika. v. Kuwa tayari asubuhi ya Shule ya Sabato ……
3. Kiongozi Msaidizi wa Shule ya Sabato – Uinjilisti Baadhi ya majukumu yake:
i. Kusimamia uinjilisti wa Shule ya sabato katika jumuiya ii. Kupanga na viongozi wa migawanyo na walimu kwa ajili ya shughuli za uinjilisti kupitia madarasa ya Shule ya Sabato iii. Kupanga kwa ajili ya siku za Wageni iv. Kupanga pamoja na viongozi wa migawanyo kwa ajili ya siku za maamuzi v. Kupanga na Mkurugenzi wa shule ya Sabato wakati wa likizo (VBS) kwa ajili ya program za VBS. vi. Kupanga na viongozi wa migawanyo kufungua matawi ya Shule ya Sabato vii. Kukuza ufuatiliaji kwa ajili ya wageni viii. Kuhudhuria Baraza la Shule ya Sabato na kutoa taarifa juu ya shughuli za mipango kwa ajili ya uinjilisti kwa jamii. ix. Kuwa tayari asubuhi ya Sabato …….
4. Kiongozi Msaidizi wa Shule ya Sabato – Utandaaji
Watandaaji ni washiriki ambao kwa sababu mbalimbali hawawezi kuhudhuria daima vipindi vya Shule ya Sabato. Wanaweza kuzuiwa na:-
a. Matatizo ya usafiri
b. Ugonjwa
c. Uzee
d. Hali zisizoepukika nyumbani Kiongozi huyo huchaguliwa wanapokuwepo watandaaji zaidi ya watatu. Wasipozidi watatu, hutunzwa na Karani wa Shule ya Sabato au Msaidizi.
Baadhi ya majukumu yake:
i. Hufanya kazi chini ya Kiongozi Msaidizi wa Shule ya Sabato – Ushirika ii. kuwasiliana na washiriki wasioweza kuhudhuria Shule ya Sabato iii. kuwasiliana na Mchungaji, Mzee / Wazee wa Kanisa, Msaidizi wa
Shule ya Sabato – Ushirika, na yeyote anayeweza kutoa habari za wale wanaopaswa kuandikishwa katika utandaaji. iv. Kudumisha mawasiliano na watandaaji kwa kuwatembelea ikiwezekana, au barua au simu. v. Kuhakikisha watandaaji wanapata miongozo ya kujifunza Biblia, somo la nchi za mbali, bahasha za matoleo, vifaa vingine vya Shule ya Sabato vinavyotakiwa ili wapate Baraka zote za Shule ya Sabato. vi. Kuhudhuria baraza la Shule ya Sabato na kutoa taarifa juu ya kitengo chake vii. Kutoa taarifa kamili ya watandaaji na matoleo yao kwa Karani wa Shule ya Sabato mwisho wa juma, mwezi na robo. viii. Kuwa tayari asubuhi ya Sabato ……
5. Kiongozi Msaidizi wa Shule ya Sabato – Ukarimu Baadhi ya majukumu yake:
i. Kufundisha kutoa semina, na kusimamia mabawabu / wakaribishaji. ii. Kupanga na viongozi wa migawanyo kuhakikisha kuwa somo la misheni lipo katika programu ya Shule ya Sabato. iii. Kufanya na walimu kuhakikisha washiriki wapya na wageni wanakaribishwa au kanisani. iv. Kupanga na kuhimiza programu ya kuwakarimu wageni milo, ama majumbani au kanisani. v. Kukuza mpango wa ufuatiliaji kwa wageni wote wanaohudhuria